Sunday, 20 May 2018

Chelsea imetwaa Ubingwa wa FA Mbele ya Man United

Club ya Chelsea ambayo pamoja na kupoteza nafasi ya kushiriki michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 leo imefanikiwa kuwafuta machozi mashabiki wake kufuatia kupata ushindi wa FA mbele ya Man United katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA katika uwanja wa Wembley.

Chelsea leo imefanikiwa kutwaa Ubingwa huo kwa kuifunga Man United kwa goli 1-0, goli pekee la Chelsea likigungwa na Eden Hazard dakika ya 22 kwa mkwaju wa penati na kuwafanya Man United wakiondoka Wembley vichwa chini.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM