Tuesday, 29 May 2018

Ajali ya bodaboda yaua Familia

Watu watatu wa familia moja wamefariki dunia papo hapo katika ajali iliyohusisha pikipiki na basi mali ya kampuni ya Saratoga.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema tukio hilo limetokea leo, Mei 29 saa 6 mchana katika eneo la kituo cha mafuta cha Munio, mjini hapa.

Amewataja wanafamilia Marehemu hao ni wakazi wa kitongoji cha Katandala mjini hapa.

Kamanda Kyando amesema kuwa ajali hiyo ilihusisha basi la kampuni ya Saratoga lenye namba T 211 AED aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na Ally Fabiano (31) mkazi wa Kigoma.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM