Monday, 11 December 2017

WATU WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI LA MUME WA ZALI, BILIONEA IVAN SSEMWANGA UGANDA


Maafisa wa usalama nchini Uganda wameanzisha uchunguzi kubaini nani waliokaribu kufukua kaburi la Ivan Ssemwanga.

Gazeti la serikali la New Vision linasema Ivan Ssemwanga watu wasiojulikana walichimba shimo kwenye kaburi la Ivan katika kijiji cha Nakaliro, mjini Kayunga Jumanne usiku.

Taarifa zinasema walichimba kutoka pembeni lakini hawakufanikiwa kulifikia jeneza.

Mfanyabiashara huyo, ambaye ni mume wa zamani wa mke wa msanii mashuhuri wa Tanzania Zari Hassan, alizikwa Mei mwaka huu katika mazishi ya 'kifahari'.

Wakati wa mazishi yake, waombolezaji walionekana wakimwaga mvinyo kwenye jeneza na pia kurusha noti za pesa ndani ya kaburi.

Marafiki wa Ivan walionekana wakirusha pesa ndani ya kaburi wakati wa mazishi

Haijabainika ni kiasi gani cha pesa zilizozikwa lakini inaarifiwa kwamba silikuwa noti za shilingi za Uganda, rand za Afrika Kusini na dola za Marekani.

Ssemwanga aliyefariki akiwa na miaka 39 alifahamika sana kwa kupenda raha sana na burudani.

Alikuwa kiongozi wa kundi lililojiita Rich Gang, kundi la wanaume matajiri Uganda.

Taarifa zinasema polisi walilinda kaburi hilo kwa mwezi mmoja baada ya mazishi hayo kufanyika.

Naibu mkuu wa wilaya hiyo Yahaya Were amenukuliwa na New Vision akisema uchunguzi umeanzishwa na kwamba washukiwa watakaokamatwa watapelekwa kortini kwa „kuvuruga amani ya wafu".

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM