Sunday, 17 December 2017

Mbunge amtaja aliyetaka kumuua Lissu

Mbunge wa Serengeti, Marwa Ryoba Chaha (CHADEMA) amefunguka na kutaja sifa za mtu ambaye alitaka kumuua Tundu Lissu na kusema mtu huyo alishindwa kutekeleza hilo kwa kuwa Mungu hakupanga Lissu aondoke kwa kipindi hicho

Marwa Ryoba amesema hayo kupitia mtandao wake wa Facebook baada ya kuweka picha ya Tundu Lissu akiwa hospitali ya Nairobi Kenya na kusema kuwa Mbunge huyo sasa anaendelea vizuri baada ya kutolewa risasi 16 mwilini. 
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma, baadaye alisafirishwa na kupelekwa nchini Kenya jijini Nairobi ambapo mpaka sasa anapatiwa matibabu huko.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM