Monday, 11 December 2017

DR. LUIS SHIKA AFANYA BALAA KUBWA KWENYE USIKU WA “900” ITAPENDEZA ZAIDI DAR LIVE!!December 9 2017 ulikua USIKU WA 900 ITAPENDEZA ambapo Mgeni rasmi alikua Dr. Shika, Mtanzania aliejipatia umaarufu kwa kugombania kununua nyumba za BILIONI 2 kwenye mnada wakati hakuwa na hata senti 5 mfukoni.
Lewis Mbonde TV na Lewis Mbonde Blog zilikuwepo kunasa kila kilichotokea kwenye usiku huu ambapo Mshonaji wa Suti aliyokua amevaa Dr. Shika alisema pamoja na viatu gharama yake ni shilingi milioni moja… tazama hii video kumuona Dr. Shika alivyotokezea.

Pia Staa wa vichekesho Bongo, Ebitoke pamoja na ‘bilionea’ aliyejizolea umaarufu baada ya kuibuka mshindi katika mnada wa nyumba za mfanyabiashara maarufu, Said Lugumi, Dk Louis Shika usiku wa kuamkia leo, waliuteka Uwanja wa Taifa wa Burudani Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar baada ya kupokea shangwe za kutosha kutoka kwa mashabiki.
Katika usiku huo uliokwenda kwa jina la Usiku wa Itapendeza, Dk Shika aliongea na wakazi wa jiji la Dar kuwaelezea maisha yake kiurefu jambo lililowasisimua wengi waliojitokeza na wengine kushindwa kuzuia hisia zao na kutoa vitambaa na kujifuta machozi.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM