Sunday, 9 July 2017

Prof Jay Ameyasema Haya Baada ya Kufunga Ndoa


Msanii wa muziki, Professor Jay amefunga ndoa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph la Posta jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 08, 2017 na mpenzi wake wa siku nyingi Grace Mgonjo.

Cherekochereko za tukio kubwa la Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule almaarufu Profesa Jay limetikisa Jiji La Dar baada ya kufuatiliwa na watu wengi. Ndoa ya Profesa Jay na mpenzi wake wa muda mrefu.

Kabla ya ndoa hiyo iliyoibua shangwe kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofurika kanisani hapo, msafara wa kuelekea kanisani ulianzia nyumbani kwa Profesa Jay, Kimara-Temboni jijini Dar.

Ndoa hiyo ilifuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo waalikwa walipata nafasi ya kula, kunywa hadi kusaza huku shughuli nzima ikipambwa na mahudhurio ya mastaa kibao wa Bongo.

“Namshukuru Mungu nimetimiza ahadi ya ndoa kwa mchumba wangu ambaye tumepitia mabonde na milima,” alisema Profesa Jay baada ya kutoka kanisani hapo.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM