Monday, 9 January 2017

Waziri Nchemba, Usikomee Kwa Chid Benz, Kuna Wengine Siyo Maarufu Ila Wako Majumbani na Mitaani

Niliwahi kuona Mh Jakaya Kikwete akijitolea kugharimikia matibabu ya Ray C ambaye wakati huo alikuwa ktk hali mbaya kutokana na kuathiriwa vibaya na matumizi ya madawa ya Kulevya. Binafsi nilimuona Ray C kama mwenye bahati kwa kitendo cha Rais kujitolea kumsaidia kupata matibabu tena nje ya nchi. Lakini baadae tunajua kuwa mwanadada Ray C alirejealea kuyatumia tena madawa hayo

Lakini ni ukweli usiopingika kuwa, wakati huo huo kulikuwa kuna watanzania wengine wengi sana waliokuwa wameathirika na matumizi ya madawa ya kulevya ambao nao wangehitaji msaada kama alioupata Ray C lakini hawakuupata na huenda hawataupata kamwe maana hawakuwa maarufu.

Hivi majuzi nimesoma taarifa zinazosambaa ktk mitandao ya kijamii kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh Nchemba amemtembelea mama yake Chid Benzi ili kuona namna anavyoweza kumsaidia Chid kutokana na matatizo anayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya. Simuonei wivu Chidi Benzi ikiwa atapata aina hiyo ya msaada maana haitakuwa mara ya kwanza Chid kupewa aina hiyo ya msaada na wasmli wema.

Lakini wasiwasi wangu ni kuwa wajibu wa serikali kuoitia mawaziri wake na Rais wake ni kuhakikisha kuwa wanawalinda watanzania dhidi ya hatari hii ya madawa ya kulevya kuingia nchini na jata kudhibiti matumizi yake.

Pia ni mategemeo yangu kuona mawaziri wa serikali wakitafakari na kuja na mpango mkakati mbadala utakaoweza kuwasaidia wale wote ambao wameathiriwa vibaya na matumizi ya haya madawa ya kulevya badala ya kulifanya hilo kama hisani kwa mtu mmoja mmoja ambaye ni maarufu pekee.

Kinachofanyika sasa hasa ktk suala hili la madawa ya kulevya, naona viongozi wanahangaika na matokeo ya tatizo badala ya kushughulikia kiini cha tatizo. Huu ni udhaifu ambao unaweza kuwanufaisha wale watakaobahatika kufikiwa lakini utakuwa umewaangamiza wengine ambao ninaamini Mwigulu hawezi kuwafikia maana siyo maarufu kama Chid Benzi

Ray C, Chid Benzi, TID na wengine wawe kama sample ya kutusaidia kujua ukubwa wa tatizo tunalokumbana nalo. Ikiwa tunawasaidia mmoja mmoja basi tuweke na utaratibu mwingine wa wazi wa kutembelewa na Waziri wa serikali ili kujadiliana na familia zote zenye watu wa aina hii namna nzuri ya kuwasaidia. Kama hilo haliwezekani basi ni wajibu wa serikali kuweka mikakati ya wote wenye tatizo hili kupata usaidizi.

Mh Mwigulu kama kweli unataka kusaidia huu ni muda wa Kuishauri Serikali kupitia baraza la mawaziri namna gani tatizo hili linaweza kushughulikiwa kwa kuweka mipango ya muda mrefu, na mipango ya muda mfupi bila kusahau mpango mkakati wa kupatikana kwa vituo (Sober House) vya kuwasaidia waathirika hawa kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya ktk maeneo ya yaliyoatjirika zaidi kama Pwani , Dar, Zanzibar nk

Mh Mwigulu wewe ni Waziri wa Mambo ya Ndani, andaa mikakati yenye matokeo chanya kwa kushirikiana na mamlaka nyingine ili Tanzania iwe mahala salama dhidi ya dawa za kulevya.

Magoiga SN

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM