Monday, January 2, 2017

WAKAZI WA LOS ANGELES WAANZA MWAKA MPYA NA SUPRISE YA “HOLLYWEED”

Kama kawaida kila tunapofunga mwaka au kuuanza mwaka lazima tutakutana na watu wenye vituko kwa ajili ya kushangaza jamii, Mwaka 2017 mpya na Hollywood imebadilishwa imekuwa Hollyweed.

Wakazi wa Los Angels waliamka na Suprise ya kufa mtu siku ya mwaka mpya baada ya sign kubwa ya “Hollywood” kubadilishwa na mtu asiyejulikana na kusomeka “Hollyweed”.
Tukio hili la kubadilishwa kwa nembo hii ya Hollywood kuwa Hollyweed linadaiwa kufuata mwangwi wa jamaa mmoja  alikuwa anajulikana kama Danny Finegood ambaye ni marehemu, miaka 41 iliyopita aliwahi kuibadilisha nembo hiyo yeye pamoja na marafiki zake  Jan. 1, 1976.
Ishu ya kubadilisha nembo hiyo ya “Hollywood” kuwa “Hollyweed” ilianza pindi California ilipolegeza kwenye sheria ya Marijuana, hakuna ushahidi wa kutosha kama tukio hili la 2017 linamaana sawa na hilo la 1976.
Licha ya kufanikiwa kuirekebisha polisi bado wanaendelea kufanya uchunguzi kwa mtu ambaye amehusika na tukio hilo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.