Friday, 6 January 2017

Tazama picha za Jennifer na Patrick wa Kanumba alioigiza nao kwnye UNCLE JJ walivyokua wakubwa

Watu wengi watawakumbuka Jennifer na Patrick kwa jinsi walivyoweza kutikisa tansia ya filamu Tanzania kipindi cha nyuma walipoibuliwa na marehemu Steven Kanumba.

Watoto hawa wawili walicheza kwa ustadi mkubwa katika filamu za Uncle JJ na This is It zote za marehemu Kanumba.

Kwa sasa Hanifa Daud ‘Jennifer’ na Othman Njaidi ‘Patrick’ si watoto tena. Wawili hawa hawajaonekana sana kwenye filamu baada ya Steven Kanumba aliyewatoa kufariki.

Jennifer ambaye amehitimu kidato cha nne mwaka jana mara ya mwisho alionekana kwenye filamu ya Zena na Betina ya Salma Jabu a.k.a Nisha mwaka 2014. Kwa upande wake Patrick, yeye alisema kuwa hana shauku ya kuigiza tena kama ilivyokuwa awali.
Credit: Bongo5

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM