Thursday, 12 January 2017

Rais Magufuli: Msidanganywe patakuwa na chakula cha msaada, serikali haina shamba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametoa wito kwa wakazi wa maeneo mbalimbali nchini kutumia mvua zinzoendelea kunyesha kwaajili ya kulima mazao yanayostahimili ukame baada ya kutegemea chakula kutoka serikalini.
Hayo ameyazungumza alipowasili eneo la Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza kutokea Chato mkoani Geita huku akipokelewa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mwanza wakiongozwa na mkuu wa mkoa.
“Ninafahamu wapo wanasiasa wachache ambao wanafikiri mzee bure, kila kitu kikitokea serikali ifanye, serikali ninayoiongoza mimi haitatoa kitu, mlinichagua niwaeleze ukweli na mimi nawaeleza ukweli,” alisema Magufuli.
“Sasa hivi wakati wa kulima mahindi umebadilika, tusijilazimishe kulima mahindi ambayo yanahitaji mvua nyingi mvua zinaponyesha tulime, na asiye fanya kazi na asile, msije kamwe mkadanganywa na mtu yeyote kwamba patakuwa na chakula cha serikali nataka niwaambie hakuna shamba la serikali,” alisema.
“Nani anaweza akanionyesha shamba la serikali, hakuna shamba la serikali, mlinichagua niwaambie ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli ni lazima tufanye kazi tujipange,” aliongeza
BY: Emmy Mwaipopo

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM