Tuesday, 3 January 2017

NIKKI MBISHI AMLILIA NANDO BAADA YA AFYA YAKE KUZOLOTA KWA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA


Siku chache baada ya kuandika message yake kuhusu afya ya rapa Chid Benz ambaye ameathirika na matumizi ya dawa za kulevya ambazo inaelezwa amekuwa akizitumia kwa muda mrefu pamoja na kupelekwa Rehab lakini bado amerudia tena, nimekutana hii nyingine ya Nikki Mbishi kuhusu Nando, mshiriki wa “BBA The Chase”.

Hivi karibuni mshiriki huyo wa Big Brother Africa msimu wa The Chase amekutwa akiwa kwenye hali mbaya kiafya kwa kile kinachoelezwa ni kuzidiwa na dawa za kulevya. Nikki Mbishi ameandika maneno ya kuonesha kutofurahishwa na kile Nando amekuwa akikifanya.
Hiki kimeandikwa na Nikki Mbishi kupitia Instagram.
#NANDO stop whatchu doin bruh,get off whatchu on to! I’d like to see u this effectively healthy. Hatua uliyofikia ulipaswa kuwa mfanya biashara mkubwa due to the huge exposure you got for reppin’ yo country in #BBA. Come back to the essence of time home boy.
Mkono wa Mungu na ukuguse na usisite kugeuka ukiguswa,sipendi picha zako zinazosambaa mitandaoni,jifunze kupitia kaka zako waliopotea kwenye hayo mambo. #UNLUCKY_ME Most of my friends are unfortunately dragged into drugs but why GOD? Be Blessed and happy new year! – Nikki Mbishi

Nando anavyoonekana baada ya kuzidiwa na dawa za kulevya
2058426_3695782

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM