Thursday, 12 January 2017

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA ARIPOTI SHULENI KWA CHOPA
Shughuli za masomo zilisimama kwa muda shule ya Nyeri High School nchini Kenya Jumatano asubuhi wakati mwanafunzi aliyeripoti kuanza elimu ya kidato cha kwanza alipotua kwa chopa.
Kijana Kevin Muriuki, aliyepasi katika shule ya msingi ya Karichen alipelekwa shuleni hapo kwa njiamya anga na chama cha veterani wa kikosi cha anga cha Kenya (Kenya Air Force Veterans Association).
Muriuki, anayetoka kwenye familia inayoishi kwenye mazingira magumu, ana ndoto ya kuwa rubani wa ndege na maveterani hao wakaona wamwonjeshe kwa kumpeleka shuleni kwa chopa.

Kijana Kevin Muriuki na chopa iliyompeleka shuleni Nyeri

Kijana Kevin Muriuki na wazazi wake wakielekea kwenye chopa

Kijana Kevin Muriuki akiaga

Kijana Kevin Muriuki haamini bahati yake

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM