Monday, 9 January 2017

Mtabiri Atabiri Vifo vya Viongozi wa Dini, Siasa, Wasanii na Wanahabari Tanzania


Mnajimu, Maalim Hassan Yahya Hussein ametabiri vifo vya viongozi mbalimbali wa kidini, kisiasa, wasanii pamoja na wanahabari kama vilivyotokea kwa mwaka 2016.

Hassan Hussen ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam kuhusu utabiri wake wa mambo mbalimbali yatakayotokea mwaka huu.

Akiwa katika mkutano huo alitaja baadhi ya mambo ambayo anaamini yatatokea mwaka huu ikiwa ni pamoja na kutokea kashfa kubwa sana ya ngono au fumanizi itakayowahusu viongozi wa dini, siasa na wasanii maarufu itakayosababisha  viongozi hao kufedheheshwa  na kuanguka kabisa katika tasnia zao.

Alisema pia kuwa, viongozi wakubwa wa upinzani duniani na Tanzania watarejea kwenye vyama walivyovihama miaka ya nyuma kutokana na sababu mbalimbali. Mwaka huu pia kutakuwa na vifo vya viongozi wakubwa maarufu wa kisiasa  na kidini, baadhi ya vifo vitakuwa ni vya ghafla ambavyo vitasababishwa na msongo wa mawazo na shinikizo la damu.
Vifo vya vya ghafla vya wasanii maarufu duniani ikiwemo Tanzania vinaweza vikatokana na fumanizi au kuuliwa au kuana wenyewe.

Pia alisema moto mkubwa utatokea nchini na duniani.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM