Saturday, 7 January 2017

MOHAMED TRANS YAPATA AJALI MBAYA SINGIDA,WATU KADHAA WAFARIKI DUNIA


Nimepita hapa kidogo kabla ya kufika Manyoni nimekutana na hii ajali mbaya. Inadaiwa watu 3 wamefariki na majeruhi ni 6. Aidha, inasemekana ni walimu ambao walilikodi basi kutoka Tanga.Chanzo cha ajali ni gari ndogo lililokuwa
limeegesha barabarani bila tahadhari, mbele ya basi kulikuwa kuna lori la mafuta hivyo dereva wa lori alipoona mbele kuna gari imepaka na yeye akatanua kwa haraka.Wakati huo basi nalo lilikuwa linataka ku-overtake hivyo dereva wa basi akashindwa kulimudu kutokana na mwendo kasi na akaligonga roli la mafuta kwa nyuma na kutoboka kitu kilichopelekea kumwagika mafuta barabarani.
Tushukuru Mungu havijatokea vifo zaidi kwa sababu mafuta yaliyotapakaa ardhini hayakushika moto.
Mungu awaweke mahala panapostahili marehemu wote, amina.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM