Sunday, January 8, 2017

Mke wa Masele Ashauriwa Ajiandae kwa Vicheko

 BI Specioza Malick  mke wa msanii wa vichekesho nchini aliyejipatia umaarufu mkubwa kwa mtindo wake wa kuchekesha, Chrispine Lyogello ‘Masele Chapombe’,  ni vyema akajitayarisha kucheka na kuvunjika mbavu kutokana na sanaa hiyo ambayo mumewe anaiweza ilivyo.

 Mrembo huyo, aliyefunga ndoa na msanii huyo mwezi huu wa Januari,  ameshauriwa na mashabiki wa sanaa ya mumewe ajitayarishe kucheka zaidi na wakati huohuo awe na ubavu wa kutenganisha kazi ya Masele na maisha yake halisi.

“Mke wa Masele ajiandae kucheka mpaka kuumwa mbavu siku Masele akiamua kumletea nyumbani vituo anavyofanya kwenye televisheni nyumbani.   Bi Specioza ajiandae kuwa maarufu kwani kwa sasa ameungana mwili mmoja na mtu maarufu nchini,” alisema shabiki mmoja aliyejitambulisha kama Bondi Masaba wa jijini Dar es Salaam.

Ndoa ya wawili hao ilifungwa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Consolata lililopo Mbezi-Makabe jijini Dar es Salaam.
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.