Tuesday, 10 January 2017

MKE ANYWA MAJI YA BETRI AKIMTUHUMU MMEWE KUCHEPUKA NA WANAWAKE WENGINE


MKAZI wa Kijiji cha Kimelembe wilayani Ludewa, mkoani Njombe, Maria Kayombo (31) amenusurika kifo baada ya kunywa maji ya betri kutokana na wivu wa kimapenzi.
Akizungumza jana, mama mzazi wa mwanamke huyo Magdalena Kayombo alisema tukio hilo lilitokea juzi ambapo alipigiwa simu akiwa shambani kuwa hali ya mtoto wake ni mbaya baada ya kunywa sumu.
Alisema walimkimbiza katika zahanati ya jirani ambapo alipatiwa matibabu na kumweleza kuwa alikuwa amekunywa maji ya betri baada ya kugombana na mumewe, Peter Henjewele akimtuhumua kuwa na ‘mchepuko’.
“Sikuweza kumhoji sana kwani nilishikwa na mshangao aliponiambia amekunywa maji ya betri ili afe amuache mumewe aendelee kuwa na mchepuko,” alisema.
Akizungumzia hali hiyo baada ya kupata nafuu mwanamke huyo alisema chanzo cha yeye kuchukua uamuzi huo ni kitendo cha mume wake kuwa na wanawake wengine nje.
“Tulianza nae maisha katika hali ngumu, kitendo cha kuanza kuchepuka wazi wazi na wanawake wengine ni dharau nikaona bora nife kuliko kuvumilia maumivu hayo ya kimapenzi,” alisema.


Hata hivyo, mume wa mwanamke huyo, alitokomea kusikojulikana baada ya kuona mke wake amekunywa maji ya betri.
Chanzo-Mtanzania

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM