Saturday, 7 January 2017

Max Rioba adai ameshindwa kufanyakazi na Young Dee kwa kuwa hana nidhamu

Uongozi wa label ya Millian Dollar Boys ‘MDB’ iliokuwa unamsimamia rapper Young Dee, amedai hawafanyi tena kazi na rapper huyo kwa madai rapper huyo hana nidhamu. Young Dee akiwa na boss wake wa zamani Max
Max Rioba ambaye ni mkurugenzi wa label hiyo, wiki moja iliyopita alionekana kulalamika katika mitandao ya kijamii akidai rapper huyo amerudi tena katika matumizi ya Madawa ya kulevya.
Akiongea Ijumaa hii katika kipindi cha FNL cha EATV, Max amedai habari za rapper kurudia matumizi ya Madawa ya kulevya na yeye anaziona katika mitandao ya kijamii kuhu akikiri kutofanya kazi tena na rapper huyo kwa madai ya kuwa hana nidhamu.
“Kwa sasa Young Dee hayupo tena kwangu,” alisema Max. “Sikumfukuza Young Dee kutoka kwangu, nilimwambia aondoke, kuna tofauti kati ya kumfukuza na kumwambia aondoke, sababu ni nidhamu.,”
Pia Max alidai kama rapper huyo atahitaji msaada wa pesa kutoka kwake ataendelea kumsaidia lakisi sio tena kuwa pamoja kama zamani.
“Young Dee akihitaji msaada wa kifedha nitamsaidia, hata binti aliyezaa naye akikwama kifedha mimi nitamsaidia, simchukii Young Dee,” alisema Max.
Katika hatua nyingine Max amedai kwa sasa hadhani kama atakuwa na nafasi tena ya kupokea msanii yeyote na kumsimamia.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM