Friday, 13 January 2017

MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA MAPINDUZI YALIVYOFANYIKA JANA ZANZIBAR


Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakionyesha uwezo wao wa kupigana bila silaha katika Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye wawnja wa Aman Januari 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakionyesha jinsi matofari yanavyoweza kuvunjwa juu ya kichwa katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Januari 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Komandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiwa amelala juu ya misumari huku wenzake wakipita juu yake ikiwa ni moja ya maonyesho ya ukakamavu yaliyoonyeshwa na Makomandoo hao katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman Januari 12. 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein akihutubia katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman Januari 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Karume akiteta na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Aman Zanzibar Januari 12, 2017. 
Baadhi ya waandamanaji wakishangilia wakati walipopita mbele ya Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Zanzibar Januari 12, 2017.
Mmoja wa wananchi wa Zanzibar akimsikiliza kwa makaini Rais wake, Dkt. Ali Mohammed Shein wakati alipohutuba katika Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman Januari 17, 2017.
Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sif Idd wakifuatilia kwa makini gwaride la Maaddhisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Januari 12, 2017
Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi cha Zanzibar akipita kwa ukakamavu mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika gwaride la kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, 2017.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM