Saturday, 7 January 2017

KOCHA WA CHEKA KOMANDO AVUNJA UKIMYA AFUNGUKA KUHUSU KUFUNGIWA KWA FRANCIS CHEKA


Na Lewis Mbonde Blog
Akifanya mahojiano na mtandao huu LEWIS MBONDE BLOG mapema leo Mjini Morogoro kocha wa Cheka Abdallah Salehe “Komando amefunguka mengi kama ifuatavyo:-
Mwandishi:Shikamoo mzee
Kocha:Marahaba
Mwandishi:Tupatie historia yako katika mchezo wa ngumi kwa ufupi
Kocha:Kwanza napenda kulishukuru jeshi la wananchi la Tanzania kwa kunipa mafundisho mazuri,ualimu wa ngumi ukiwa ni mojawapo,ila kwa sasa nimestaafu nipo uraiani nab ado naendelea kufundisha mchezo wa ngumi kwa sababu naupenda na upo damuni.Nilianza kufundisha ngumi za ridhaa mwaka 2002 timu ya mkoa wa Morogoro ilifanya vizuri na mwaka huo huo nikaingia katika ngumi za kulipwa na kuanza kumfundisha bondia Francis Cheka na kufanikiwa kushinda mikanda mitano (5) Taifa,UBO,WBC,WBF, IBF na kuwa bingwa wa dunia mpaka sasa
Mwandishi:Ni changamoto gani unazokutana nazo katika mchezo wa ngumi?
Kocha:Kwanza ni kwa mapromota na vyama vya ngumi baadhi ya mikataba haifuati sheria za kimikataba.Utakuta promota anaamua kumsainisha bondia mwenyewe tu pasipo uwepo wa trainer wake ambaye anakua ni shahidi pia pasipo uwepo wa Mwanasheria, TPBC na BMT.Hapo ndipo migogoro inapoanza pindi inapojitokeza tofauti.
Mwandishi:Umelichukuliaje suala la TPBC kumfungia bondia wako Francis Cheka kwa mda wa miaka 2 ?
Kocha:Nasema kwamba bondia hana chama anaweza kuchezea chama chochote cha ngumi duniani.Wamemfungia Cheka asicheze kwenye chama cha TPBC tu,lakini cheka bado anaweza kucheza ngumi kwenye vyama vingine vya ngumi hapa Tanzania ambavyo vimesajiliwa kisheria kama vile PST naTPBO.
Mwandishi: Ni kweli Francis Cheka amestaafu kucheza mchezo wa ngumi?
Kocha: Hapana hajastaafu kucheza ngumi nimemshauri aendelee kucheza ngumi maana ni kazi inayoendesha maisha ya familia yake na uwezo bado anao wapenzi wa cheka wategemee ujio mpya wa cheka mpya kuendelea kuitangaza nchi yetu ndani na nje ya nchi
Mwandishi: Nini ushauri wako kwa vyombo husika vinavyosimamia mchezo wa ngumi Tanzania?
Kocha: BMT inatakiwa kufanya uchaguzi wa viongozi wa chama cha TPBC wenye sifa za uongozi na wanaoelewa ngumi.Mapromota na wachezaji wote wasajiriwe BMT ili kuepuka migogoro
Mwandishi:Ahsante sana mzee wang Abdallah Salehe “Komando” kocha wa cheka
Kocha:Ahsante Nawe pia

LEWIS MBONDE BLOG

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM