Wednesday, 4 January 2017

KAULI HII YA NAY, INAWEZA KUWASAIDIA MASHABIKI KUWATOFAUTISHA DIAMOND NA ALIKIBA

Kumekuwa na wakati mgumu kwa mashabiki wa muziki wa Bongo fleva kutofautisha pale linapokuja swala la Diamond Platnumz pamoja na Alikiba, kila shabiki amekuwa akivuta kwa msanii wake na kusema huyu bora, huyu mkali, huyu ndiye anayefaa, Nay wa mitego yeye amekuja kuwatofautisha kwa jambo hili.

Baada ya kuachia ngoma yake ya “Sijiwezi” ambayo inafanya vizuri kwa sasa kwenye Industry ya muziki, Nay ameamua kufunguka na kuiweka tofauti ya Diamond pamoja na Alikiba kwa kutumia jambo hili ambalo najua mashabiki wa muziki wanaweza kuungana na Nay.
Akiongea na Planet Bongo Nay amefunguka na kusema kwamba katika wasanii wakubwa watatu Tanzania wazuri wa kwanza atakuwa ni Alikiba na likija swala la Wasanii watatu wakubwa Wafanya biashara Tanzania Diamond Platnumz kwake ni wa kwanza.
“Watu wanajenga picha kuwa mimi na Alikiba siwezi kufanya naye kazi sababu tu ya uswahiba wangu na Diamond ni kweli Alikiba si mshikaji wangu lakini leo hii ukiuliza nikutajie wanamuziki watatu wazuri Tanzania wa kwanza nitamtaja Alikiba, lakini pia ukisema nitaje wasanii watatu wakubwa wafanyabiashara basi nitamtaja Diamond Platnumz” alisema Nay wa Mitego.
Niachie Comment yako hapa chini, wewe unaweza kuwatofautisha vipi Diamond Platnumz na Alikiba

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM