Wednesday, January 4, 2017

KARRUACHE AWAPA MAKAVU CHRIS BROWN NA SOULJA BOY WALIOANZISHA BIFU SABABU YAKE

Mwaka 2017 umeanza vibaya kwa Chris Brown na Soulja Boy – kwakuwa wameanzisha bifu chanzo kikiwa ni mrembo Karrueche Tran.

Bifu ya Chris Brown na Soulja Boy inayoendelea imemkera Karruache Tran na ameamua kufunguka. Wasanii hao wameendelea kutupiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuingia ugomvi ambao Karruache aliyekuwa mpenzi wa Breezy anahusishwa.
Karruache Tran
Tangu alipoachana na Karrueche Chris amekuwa akimfuatilia mrembo huyo huku mara kadhaa akigombana na wanaume ambao wanaomtolea udenda. Na sasa balaa limemkumba rapper Soulja Boy baada ya kulike picha ya mrembo huyo kwenye mtandao wa Instagram kitendo ambacho kimeonekana kumkera Brown.
Mrembo huyo ameiita drama ya wasanii hao kuwa ni ya kijinga na haina maana yoyote hata katika mwaka mpya. Amewaomba wamtoe kwenye malumbano yao.
Tazama alichokiandika pamoja na jibu la Chris Brown..
Hii inshu yote ilikuja baada ya Soulja Boy kufunguka kupitia mtandao wa Twitter kuwa Chris amemtafuta na kumpiga mikwara baada ya kulike picha hiyo.

Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.