Wednesday, 4 January 2017

KALAPINA AFUNGUKA KUHUSU YOUNG D KURUDIA MADAWA YA KULEVYA

Wiki hii habari za kumuhusu Young D kurudia
unga zilisambaa mitandaoni huku meneja wake 
Maximilian akilalamika na kuonyesha kweli msanii 
huyo kaanza kurudia matapishi yake

Kwenye planet bongo ya EA Radio Kalapina alifunguka
haya baada ya kuulizwa anampango gani yeye kama 
mwanaharakati kwa msanii huyo (young d) ikiwa bado
hayajaanza kumuathiri sana "Young D mimi nishakuwa
nae siku za nyuma nishafanya nae cancelling sana lakini
ni mtu ambaye kwanza yeye mwenyewe si mtu ambaye
anajikubali unajua, haya mambo yanataka mtu ujikubali 
kwanza wewe mwenyewe kwenye nafsi yako" alisema
kalapina "Ukikutana nae sasa hivi young D anakataa 
atakuambia aah stant tu, lakini ukimuona unaona kabisa
huyu mtu mbona hasomeki
.
.

Hata hivyo @dullahplanet mtangazaji wa kipindi hicho cha planet
bongo alikazia na kumtaka @kalapina amsaidie Young D
kabla hajaathiriwa sana "Sasa inafaa umtafute mapema 
zaidi kwasababu taarifa zinasema amerudi, kwasababu 
tunapata uwezo wa kusema hivyo kwa maana page ya 
instagram ya meneja wake amekuwa akilalamika na ameonyesha 
haitaji tena kumsaidia anaona kama anapoteza muda hivi, 
kwasabubu inasemekana dogo alikuwa akiagiza msosi usiku 
vyombo (madawa ya kulevya) alikuwa anaviweka chini ya chipsi 
yani chipsi zikija vyombo vinapigiliwa kwa chini halafu juu kiepe 
kinakaa kwahiyo mlinzi akipewa mfuko ile anapeleka anajua oya 
oya kumbe kaweka vitu ndani"

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM