Thursday, 12 January 2017

Izzo Business Aeleza Jinsi Alivyosaidiwa na Chid Benz Kifedha na Kimuziki
Nimewahi kuzungumza na Ditto kwa ufupi na akanieleza kuwa katika watu wenye roho nzuri katika kusaidia watu, Chidi Benz ni namba moja.

Alisema kipindi ambacho rapper huyo ana fedha, washkaji wengi wa karibu yake walifaidika sababu hana tabia ya uchoyo. Izzo Bizness amekiri kuwa mmoja wa watu walionufaika na ukarimu wa Chidi Benz.

“Hata mimi wakati sina kitu yaani, unakuta unampigia simu ‘ebana eh inakuaje uko wapi? Hebu njoo tukutane Ubungo.’ Unaenda unachezea labda shilingi 50 fulani, shilingi 30,” alisema @izzo_biznesss kwenye mahojiano na kipindi cha The Playlist cha @timesfmtz.

Izzo anadai kuwa pamoja na misaada ya kifedha ya hapa na pale, Chidi alikuwa mtu aliyekuwa akimpa ushauri mwingi uliomjenga kimuziki.

“Chidi atabaki kuwa big brother, kuna mambo ya duniani kila mtu ana mitihani yake lakini hata mimi namuombea, nammiss, game imepoa Chidi ni bonge ya rapper, hamna ambaye hajui, kuna vijana wengi sana ametusaidia,” amesisitiza Izzo biznesss.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM