Wednesday, January 4, 2017

HILI ni jibu la Diamond kuhusu kwanini anataja majina ya wacheza soka kwenye ngoma zake


Sio kitu cha ajabu kusikia wasanii wakiwarusha wanamichezo kwenye ngoma zao. Hiki kitu kimeanza muda mrefu sana ndani ya Africa hadi nje ya Africa. Mmoja kati ya wanamichezao waliohi kutajwa sana kwenye nyimbo za HipHop huko marekani ni Michael Jordan au M.J kama wanavyomuita.

Tumeongea na Diamond Platinumz ambapo yeye na wasanii wake wa WCB wamekua wakitaja majina ya wana michezo mara kadhaa kwenye ngoma zao hasa Ronaldo na Mbwana Samatta.

Diamond tulipomuuliza kuna faida gani kwake na kipi kinamvutia kutaja majina ya wachezaji hao kwenye ngoma zake. Jibu lilikua hili “Hata kama mtu anafanya kazi kiasi gani kama jamii haijamkubali basi bado ana kazi ya ziada ya kufanya hadi akubalike.”

Aliendelea “Sasa mimi nawataja watu ambao wamefanikiwa kukubalika na jamii, ukiangalia watu kama Ronaldo na Samatta inaongeza chachu ya nyimbo na kupendwa zaidi. Hata wao pia wanafarijika kuona kwamba sisi kwa sisi pia tunakubaliana kwa kila kitu tunachofanya.
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.