Wednesday, January 4, 2017

HIKI ndicho kilichovunja ndoa ya Mkwasa na TFF


TFF limesema, kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Charles Boniface Mkwassa “Master” ni makubaliano ya kimkataba kwa pande zote mbili na hakukuwa na tofauti zozote ziliyojitokeza.

Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas amesema, wanatarajia kumalizana kabisa na Mkwasa mpaka ifikapo mwezi wa Machi mwaka huu ikiwemo fidia za kukatisha mkataba.

Alfred amesema, wataendelea kufuata program aliyoiacha Mkwasa huku wakitumia pia programu ya Kocha Salum Mayanga ambaye atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).

Mkwasa alichukua mikoba kutoka kwa kocha Mart Nooij raia wa Uholanzi ambaye alifundisha tangu mwaka 2014 hadi 2015.

Kocha Salum Mayanga anachukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi wa Machi, mwaka huu ambapo kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitaanza mapema mwaka huu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.