Friday, January 13, 2017

HII NDIO SIFA AMBAYO DUDU BAYA AMEMPATIA DARASSA

Moja ya wakongwe wakali kwenye game ya muziki wa Bongofleva hapa nchini huwezi kumuacha Dudu Baya, na katika ukongwe wake kwenye game Dudu ametoa sifa kwa Darassa.
Darassa sasa amekuwa ndio kichwa cha habari kwa kila shabiki wa muziki hapa nchini na hii ni kutokana na ngoma yake ya “Muziki” ambayo inafanya vizuri kila kona na kumletea mafanikio mengi kwenye muziki, Sasa kupitia kipindi cha Enewz cha Eatv Dudu baya alifunguka na kusema kwamba hakuna msanii mwenye heshima kama Darassa.

“Darassa ni mdogo wangu ameanza kuimba muda mrefu sana lakini saizi ndiyo ametoboa, kile alichoimba sijui siyo Kenge siyo Simba siyo Mamba zile ni fleva tu za muziki amepiga mistari na mimi ngoma yake nai support. Lakini niseme tu hakuna msanii mwenye heshima kama Darassa narudia tena hakuna msanii mwenye heshima kama Darassa” Alifunguka Dudu Baya.
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.