Friday, January 13, 2017

Darasa Akiri kuwa Aliwahi Kwenda Kwa Sangoma ili Afanikiwe Kimuziki

http://4.bp.blogspot.com/-1IR3NcfH5Mg/Vp_ei3LZHUI/AAAAAAAAGRY/UbNpm0Q9K3w/w1200-h630-p-nu/DARASSA.jpg
Mwanamuziki wa bongofleva nchini Tanzania anayefanya vizuri na wimbo wake wa Muziki, Darassa kwa mara ya kwanza amekiri kuwa aliwahi kwenda kwa mganga wa kienyeji ili amsaidie atoke kimaisha.

Darassa aliyasema hayo jana usiku alipokuwa katika kipindi za Ala za Roho cha Clouds Fm ambapo mtangazaji alitaka kujua kama aliwahi kwenda kwa mganga tangu azaliwe.

Nimewahi kwenda kwa mganga mara moja, ni kipindi cha nyuma kidogo. Nilikwenda kwa mganga baada ya maisha kuwa magumu sana nikiamini ataweza kunisaidia. Unajua mimi nimekulia uswahilini na kule ukiwa kijana kunakuwa na mambo mengi sana, hivyo nilishawishiwa nikakuta nimeenda, alisema Darassa.

Darassa alisema baada ya kufika kwa mganga aliona kuwa mganga hawezi kumsaidia na tangu alipoondoka hakurudi tena. Aidha, alisema kuwa aliacha kuamini kwenye masuala ya kishirikina kwani ndio kikwazo kikubwa cha wakazi wengi wanaoishi uswahilini hawaendelei.

Darassa amewaasa watu mbalimbali wanaoamini katika imani za kishirikina kuwa hazitawasaidia na badala yake Mungu yupo na wakimuamini atawasaidia kama ambavyo imekuwa kwake ambapo ametoka kwenye maisha ya dhiki sana.

Alipoulizwa kama ajali yake iliyotokea mwezi uliopita aliuhususha na kulogwa, alisema kuwa yeye hakuihusisha na imani za kishirikina na kuwa sababu kubwa ya ajali ni uchovu tu licha ya baadhi ya watu kusema kuwa na mambo ya kishirikina.
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.