Tuesday, December 13, 2016

YOUNG D 'Kwa Mara ya Kwanza Nimejisikia Tofauti Sana Baada ya Kumbeba tu Mwanangu'

Rapper Young Dee amesema kupata mtoto kumempa furaha ambayo hawajawahi kuwa nayo katika maisha yake.

Young amesema:

Kwa mara ya kwanza nimejisikia tofauti sana baada ya kumbeba tu mwanangu. Yaani nimejisikia tofauti hali ambayo sijawahi kuisikia wala kutegemea nitaisikia. Kwahiyo ni feeling mpya kabisa, yaani amenifanya nimepata kitu ambacho sijawahi kuwa nacho, nimepata kama nguvu hivi. Amenipa kila sababu ya kuamka asubuhi kwa kumfikiria yeye, chochote ambacho nakipata kinaenda kwa yeye. Yaani mpaka sasa hivi ameanza kubadilisha ratiba zangu, yaani kuna lifestyle ambayo naweza kuona ameshaweza kunibadilisha kwasababu kuna vitu ambavyo sivioni tena kuwa na umuhimu. Kuhusu uhusiano na mama yake ni uhusiano ambao uko vizuri sana sababu ni wa muda mrefu sijawahi kuacha kuwasiliana naye. Kwahiyo na hivi mtoto amezaliwa, nina uhakika utaimarika zaidi.

Mtoto wa Young Dee ni wa kike na anaitwa Tamar.
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.