Wednesday, December 21, 2016

WOLPER AMCHOMESHA "MAHINDI" MPENZI WAKE HARMONIZE


Katika hali inayoonyesha amekufa ameoza, nyota wa Bongo Fleva kutoka Kundi la WCB, Rajab Abdulhan maarufu kama Harmonize, ‘alichomeshwa mahindi’ kwa zaidi ya saa moja, akimsubiri mpenziwe, Jacquline Wolper aliyekuwa akila raha ndani ya pati katika Ukumbi wa Catalunya, uliopo Mwenge jijini Dar, Jumapili iliyopita.
Baadhi ya waigizaji waliokuwemo ndani ya ukumbi huo, walisikika wakisema kuwa Wolper alilalamika kuitwa na mpenzi wake Harmonize, aliyekuwa nje akimsubiri akimtaka waondoke, wakati mwenyewe alikuwa bado na hamu ya kuendelea kuponda raha.
Wakati mwanamuziki huyo akiendelea kusubiri, Wolper alikuwa akicheza na kupiga stori na baadhi ya mastaa wenzake huku akionekana kulalamika kwamba alikuwa akisubiriwa nje, hivyo wamuache aondoke.
“Jamani Harmonize atachukia sana, amekuja muda mrefu hebu niacheni niondoke, halafu unajua yule ana hasira sana,” alisikika akisema Wolper.
Nje ya ukumbi, baadhi ya watu waliokuwa nje, wakiwemo madereva wa bajaj, walisema wamemuona muda mrefu muimbaji huyo akiwa ndani ya gari bila kushuka, wakiamini anamsubiri Wolper.
“Jamani huyo Harmonize kweli kakamatika kabisa, hapa kaja zaidi ya saa moja kapaki gari tu nje, anampigia Wolper atoke lakini hatoki ndani,” alisikika akisema mtu mmoja aliyekutwa na paparazi wetu nje ya ukumbi, huku mwimbaji huyo wa kibao cha Matatizo akiwa ameshaondoka.
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.