Monday, December 19, 2016

Sungura Amtikisa Mbatia .....Amtaka Ajiuzulu Nafasi ya Mwenyekiti NCCR-Mageuzi ili Kukinusuru Chama

Aliyekuwa  Mkuu wa Idara ya Kampeni ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura, amenzisha fukuto kwa kumtaka Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia kujiuzulu nafasi yake kwa madai kuwa ameshindwa kukiongoza chama hicho tangu alipoingia madarakani.

Sungura anasema bila kufanya hivyo, atashirikiana na wanachama wengine kumwondoa, kwa sababu amekisahau chama na kujikita katika shughuli nyingine zisizo na tija, jambo ambalo limechangia chama hicho kupata mbunge mmoja kwenye uchaguzi uliofanyika Oktoba, mwaka jana.

Anasema hali ilipofikia hivi sasa, chama hicho kinaweza kufa na kubaki historia ambayo haiwezi kuwasaidia wanachama wengine wanaopigania uhuru na demokrasia ndani ya nchi yao.

“Hatumwondoi Mbatia kwa sababu tunamchukia, bali tunamwondoa kwa kushindwa kuangalia masilahi ya chama na kujikita kwenye shughuli zisizo na tija, jambo ambalo limechangia kupoteza wabunge na kubaki na mbunge mmoja ambaye ndiye yeye katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana.

“Kwa sababu nafasi ya uenyekiti si ubatizo na wala si kiungo cha mwili wake, hata tuseme tutamuumiza, hivyo basi tunaamini vijana wenye mapenzi mema na chama wataungana na mimi kuhakikisha kuwa mwenyekiti anatoka madarakani ili tuweze kukiendesha chama,”- Sungura.

Anadai  kuwa lengo lao ni kufanya siasa zenye tija, zikiwamo za kuzunguka mikoani kutafuta wanachama wapya na kuandaa viongozi ambao wataweza kukisimamia chama hadi uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

Anasema kutokana na hali hiyo, nafasi yake itakabidhiwa kwa mwanachama mwingine kama alivyonyang’anywa mwenzake na kijiti kukabidhiwa yeye ili aweze kukiongoza chama.

Sungura alijunga na chama hicho tangu mwaka 1992, akiwa mwanachama mwenye kadi N0. 00011763.

Ofisa Utawala wa chama hicho, Frolian Mbeo, alipoulizwa kuhusu kauli ya Sungura, alisema hadi jana mchana hakuwa na taarifa yoyote ya kuwapo malalamiko ya mwanachama huyo.

Alisema uamuzi wa Sungura, umekuja  baada ya kutolewa kwenye nafasi ya ukurugenzi wa kampeni, jambo ambalo limemfanya kuzunguka mikoani na kuanza kukisema vibaya chama.
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.