Saturday, December 31, 2016

Radi na ajali ya basi vyaua watu wanne SINGIDA na RUKWA

Watu wanne wamekufa na wengine 28 kujeruhiwa katika matukio tofauti yaliyotokea mikoa ya RUKWA na SINGIDA.
Picha ya Mtandao, RADI
Watu wanne wamekufa na wengine 28 kujeruhiwa katika matukio tofauti yaliyotokea mikoa ya RUKWA na SINGIDA.

Katika tukio la kwanza watu wawili wamekufa na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi kufuatia mvua iliyonyesha ikiambatana na na upepo mkali katika kijiji cha KISUMBA manispaa ya SUMBAWANGA mkoani RUKWA.

Mkuu wa wilaya ya SUMBAWANGA Dkt HALFANY HAULE amesema kamati ya maafa ya wilaya itakwenda kwenye kijiji hicho kufanya tathmini ya hasara iliyosababishwa na mvua hiyo iliyonyesha kwa dakika 40 pamoja na kutoa msaada kwa waathirika.

Katika tukio la pili watu wawili wamekufa papo hapo na wengine 26 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka KIOMBOI mkoani SINGIDA kwenda DSM kupinduka katika eneo la TUMULI.

Mganga mkuu wa mkoa wa SINGIDA, Dkt JOHN MWOMBEKI amethibitisha kupokea maiti wawili wa ajali hiyo
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.