Wednesday, December 21, 2016

NAY WA MITEGO: NITAMSAIDIA CHID BENZ NIKISHINDWA BASI.

Hitmaker wa wimbo mpya wa Sijiwezi, Nay wa Mitego amefunguka kuwa yupo kwenye mipango ya kumsaidia rapper Chid Benz kutoka kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.


Rapper huyo amekiambia kipindi cha Dj Shows cha Radio One kuwa anajaribu kumsaidia Chid lakini akishindwa basi haitokuwa bahati yake.
“Nadhani tuwaombee watu mabaya tuwaombee kwa mazuri arudi kwenye amani kama ilivyo kwa kila binadamu anayeishi tuombe heri. Chid na yeye anahitaji sana msaada. Unajua kitu amabacho mimi nimekigundua tusiwe na tabia kwamba mtu anapopotea au tunapompoteza duniani kabisa hayupo ndio tunaanza kumsifia kuwa alikuwa mkali,” amesema Nay.
“Mimi nataka kujaribu, nataka kuthubutu nikishindwa basi lakini namuomba Mungu iwe vile ninavyofikiria. Lakini sidhani kama ni kitu ambacho nakifikiria sana ila napenda kuona siku moja Chid anarudi katika hali yake. Nimekutana naye mara mbili na nimekaa naye tumezungumza nadhani anahitaji msaada sana, tena sana kwa hali na mali hasa watanzania wamuombee Chid anahitaji msaada,” ameongeza.
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.