Monday, December 12, 2016

Mzee wa Upako “Kila mwandishi aliyeniandika vibaya ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri nafunga virago nakwenda kuuza gongo"

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu Mzee wa Upako amesema waandishi wote wanaoandika habari za kumchafua watakufa kabla ya kufika Machi mwakani.

Kauli hiyo aliitoa jana ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yaliyoandikwa kwenye vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa.

“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mpo humu mmekuja na mnasikiliza tu,” alisema.
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.