Thursday, 15 December 2016

Mtoto wa Rais auawa kwa kupigwa risasi

Mtoto wa kike wa Rais wa zamani nchini Msumbiji, Armando Guebuza, Valentina Guebuza ameripotiwa kupigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Maputo. Mumewe, Zofino Muiuane amekamatwa na polisi kufuatia tukio hilo lililofanyika Jumatano.
Bi Guebuza alikua na umri wa miaka 36 na imeripotiwa alipigwa risasi mara kadhaa nyumbani kwake na kufariki dunia kutokana na majeraha wakati akipelekwa hospitalini.Mumewe alikamatwa katika moja wapo ya maeneo ya burudani mjini Maputo, kwa mujibu wa gazeti moja.
Valentina Guebuza aliorodheshwa nafasi ya saba miongoni mwa wanawake chipukizi wenye ushawishi Barani Afrika na jarida la Forbes mwaka wa 2013. Alishikilia nafasi ya juu katika kampuni kadhaa za mawasiliano pamoja na biashara zinazomilikiwa na familia.
Mumewe bwana Muiuane ni mfanyibiashara na aliwahi kufanya kazi katika kampuni ya sigara ya ‘British American Tobacco’. Wawili hao walifunga ndoa mwaka wa 2014 kwenye sherehe iliyohuhduriwa na wageni 1,700 akiwemo Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Mfalme wa Zwaziland Mswati wa Tatu na binti wa Rais wa Angola Isabel dos Santos. Walijaaliwa na mtoto wa kike mwaka uliopita. Armando Guebuza alistaafu kama Rais mwaka wa 2014 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.

Chanzo:Bongo 5

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM