Friday, 16 December 2016

MMILIKI wa Jamii Forums Apandishwa Kizimbani Kisutu, Ashindwa Kutimiza Masharti ya Dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jamii Media Limited, inayomiliki mtandao wa kijamii wa Jamii Forum (JF), Maxence Melo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi tatu tofauti lakini akasomewa mashtaka matatu.
Katika kesi hizo amesomewa mashtaka matatu, shitaka moja katika kila kesi.

Mashtaka hayo ni pamoja na kuendesha shughuli za mtandao wa kijamii bila kusajiliwa nchini na mawili ni kuzuia upelelezi.

Melo amefanikiwa kupata dhamana katika kesi mbili lakini akakwama katika kesi moja baada ya kushindwa kutimiza sharti la kupata wadhamini wawili na badala yake akampata mdhamini mmoja tu.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM