Saturday, 10 December 2016

Mchungaji awanywesha waumini dawa ya kuua bakteria “Dettol” adai ameagizwa na Mungu


Afrika Kusini inazidi kuzichukua headlines nyingine ikiwa ni wiki kadhaa tangu iripotiwe taarifa ya mchungaji aliyewapulizia waumini wake dawa ya kuua wadudu “Doom” kwa maelezo kuwa watapona magonjwa yanayowasumbua, leo nimeipata hii kuhusu mchungaji mwingine anayewanywesha watu dawa ya kuua bakteria wanaoishi kwenye majimaji “Dettol”
Mchungaji huyo maarufu kwa jina la Rufus Phala kutoka kanisa la AK Spiritual Christian lililopo Makgodu, Limpopo, Afrika Kusini amewashanga watu kwa kitendo hicho wakati ijulikana kuwa Dettol ina madhara endapo itatumika ndani ya mwili wa binadamu.
Kwa mujibu wa Daily Sun SA, mchungaji huyo alifanya kitendo hicho kwenye ibada za kawaida kanisani kwake akiwataka waumini wenye matatizo na wanaohitaji maombi wanywe Dettol aliyokuwa ameishika mkononi mwake huku akiwambia watapona shida zao ikiwemo magonjwa.
“Nafahamu kuwa Dettol ni sumu, lakini Mungu ameniagiza niwape na muitumie. Mimi nilikuwa wa kwanza kuinywa,”  – Mchungaji.
Pia amesema kuwa amepokea meseji za WhatsApp kutoka kwa watu waliokunywa na wamethibitisha kupona. Baada ya kuwepo kwa taarifa hizo, amehojiwa Daktari kutoka Afrika Kusini, Dr Mabowa Makhomisane, ambaye amekiri kuwa Dettol ina madhara inapotumika tofauti na maelekezo ikiwemo kuinywa
“Mtu akinywa Dettol na ikafika tumboni, kimsingi hupunguza mzunguko wa hewa ya Oxygen mwilini. Hali hiyo ikitokea mtu anaweza kupoteza fahamu na kufariki. “Na kama mtu atatapika na bahati mbaya maji maji yakaingia kwenye mapafu yake, Detto itamsababishia ugonjwa wa Nimonia. Mapafu yatajikunja na mtu atashindwa kupumua
Dr Makhomisane amewashauri watu waliokunywa dawa hizo waende Hospitali kupata vipimo ili kujua madhara waliyopata..

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM