Tuesday, 20 December 2016

KUELEKEA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2017 HAYA NDIO YA KUANGALIA ZAIDI KATIKA SAFARI

Picha ya maktaba gari ikiwa imepata ajali.
Na Emmanuel Kihaule
Mnaosafiri na familia kwenye magari binafsi wakati huu wa sikukuu tafadhali muwe makini. Tayari tumeshashuhudia ajali kadhaa zilizogharimu uhai na hata kusababisha majeraha makubwa.

Kumbuka kumiliki gari hakukufanyi automatically kuwa dereva wa masafa marefu! Kama huna stamina na huijiui barabara vyema basi epuka kuiweka familia yako katika hatari. Ikibidi basi endesha mchana wakati mwanga ni wa kutosha pia pata muda wa kutosha kupumzika. 
Wote waliopo kwenye gari wafunge mikanda na tabia ya kuwaacha watoto wakiwemo wakubwa kurukaruka na kucheza kwenye gari wakati wa safari ni hatari! Pia hakikisha gari imefanyiwa ukaguzi na kujiridhisha kwamba inaweza kusafiri. Je hali ya tairi, mfumo wa brake, usukani, ipo vipi? 
Pia acheni tabia ya kujazana sana kwenye magari kisa tu huyu ni mtoto wa Mjomba au shangazi hivyo hatuwezi kumuacha! Pia tabia ya kusomba kila 'takataka' kutoka nyumbani au njiani - mahindi, mihogo, viazi, maharage, nyanya, vitunguu etc. 
Mpaka kupitiliza uwezo wa gari acheni kabisa! Pia endesha kwa mwendo wa tahadhari huku ukitilia maanani alama za barabarani. Ukifanya hivyo wewe na familia yako mnaweza kuuona mwaka mpya mkiwa wazima na wenye afya badala ya kuishia mortuary au kwenye vitanda vya hospitali!

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM