Thursday, 15 December 2016

JESHI la Polisi Lafanya Ukaguzi Ofisi za Jamii Forums na Nyumbani kwa Mmiliki wa Tovuti Hiyo Maxence Melo


Leo Jeshi la Polisi limefanya ukaguzi na mahojiano kwenye Ofisi za Jamii Media(Fikrapevu.com na JamiiForums.com) na walienda pia nyumbani kwa Mwanzilishi, Maxence Melo

Polisi walichoondoka nacho ni nyaraka za usajili wa Jamii Media ikiwemo Cheti cha Mlipa Kodi, Cheti cha BRELA na Leseni ya Biashara.

Tunaomba umma utambue kwamba Jamii Media haina servers wala min-server ofisini kwake, nchini Tanzania wala Afrika. Pili, tunaomba watumiaji wa JamiiForums.com wasitiwe wasiwasi juu ya usalama wa taarifa zao.
Teknolojia tunayoitumia (encryption) kumsajili mtumiaji wa JamiiForums.com haituwezeshi kumfahamu mtumiaji yeyote labda yeye akubali kwa hiari yake kujiweka wazi mtandaoni.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM