Watu wengi walionyesha kusikitishwa baada ya habari kuenea kuwa mwanamuziki Rashid Mkwiro maarufu Chid Benz ametoroka kwenye nyumba ya matibabu (Sober house) alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya. Kwa kadiri picha zake zinavyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha dhahiri kuwa mwanamuziki huyo hali yake inazidi kuwa mbaya tofauti na alivyotoka kwenye nyumba ya matibabu ambapo aliweza kurekodi wimbo na pia kutumbuiza katika matamasha kadhaa ya muziki.
Babu Tale aliyekuwa amejitolea kumsaidia awali alisema hawezi kumsaidia tena kwani alishafanya hivyo ikashindikana na kusema Chid Benz ni sikio la kufa.
Licha ya kuwa inadaiwa kuwa hataki kupatiwa matibabu lakini ni dhahiri kuwa kwa hali yake ilivyo sasa anahitaji msaada tena wa haraka zaidi kuweza kuyanusuru maisha yake.
Hapa chini ni picha za hali ya mwanamuziki huyo kwa sasa.