Saturday, December 17, 2016

HAWA NDIO WASICHANA WATANO WALIOOTA NYWELE MWILI MZIMA

Kutana na akina dada watatu wanaotoka katika familia ya watoto sita ambao wamestaajabisha wengi huko nchini India wakiwa na sifa yakuota nywele mithili ya manyoya ya mnyama Mbweha.
Wakina dada hao ni Savita (23), Monisha (18) na Savitri Sangli (16) ambao wanaishi katika kijiji cha Pune, India na wamerithi kwa baba yao uotaji nywele huo mwili mzima.
Wataalamu wanasema kuota nywele mwili mzima yaani hata kwenye sehemu ambazo hazipaswi kuota nywele ni ugonjwa ambao kitaalamu unafahamika kama ‘Werewolf Syndrome’ ambapo seli hubadilisha mfumo na kuzifanya nywele kuota sehemu zote mwili na ni ugonjwa wakurithi.
Na kwa wasichana hao wamekuwa wakiota nywele kwa haraka sana na nyingi mwili mzima, wana ndevu lakini pia puani kwenya paji la uso na sehemu nyingine nyingi, jambo ambalo linawafanya waonekane tofauti na wasichana wengine na wengi huwashangaa na wakati mwingi huwabeza.
Hali hii imezima kabisa ndoto zao kwani wanajiona tofauti na hivyo wanaamini hawataweza kupata mambo muhimu kama wanawake wengine kama vile kuolewa, kuajiriwa, kujiremba na hata kuvaa nguo kawaida kama ilivyo kwa wanawake wengine.
Na hii inawaumiza sana kwani kwa tamaduni za kijiji chao ikiwa umefikia umri wakuolewa na ukasalia nyumbani inahesabika kama mkosi kwa mtu binafsi, familia na kijiji kwa ujumla wake.
“Wanangu hawa watatu wananisononesha sana kwani hali yao inawanyima raha na wanatafuta njia yoyote yakuwasaidia kuziondoa nywele hizo ili wawe kama wasichana wengine. Gharama yakufanya ‘surgery’ kwa kila msichana zinahitajika dola za kimarekani 7000 ambazo ni sawa na shilingi 15,250,200 za kitanzania, hivyoi jumla zinahitajika shilingi milioni 45,750,600. Na kwa bahati mbaya sina hizo pesa,” alisema mama wa watoto hao
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.