Wednesday, 21 December 2016

Hawa ndio Ma Modo 10 Waliotikisa 2016

hamisa_mobeto3
Hamisa Mobeto
Na Mwandishi Wetu|Gazeti la Ijumaa
Kwenye ulimwengu wa burudani, wapo wadada wanaofahamika kwa jina la Video Queen. Kwa hapa Bongo wapo kibao lakini katika kufunga mwaka IJUMAA linakuletea mamodo 10 waliokuwa gumzo kwa mwaka huu 2016:
Hamisa Mobeto
Moja kati ya mamodo wanaoendelea kutusua na kupata dili nyingi kutokana na muonekano. Licha ya picha zake kali kusambaa mitandaoni akitangaza mavazi, Hamisa pia mwaka huu amesumbua kupitia video za Kibongo ikiwemo Salome ya Diamond.
Gigy money (1)Mhariri wa Ijumaa Wikienda Wikienda, Sifael Paul (kushoto) akiwa na Gigy Money alipotembelea Global TV.
Gigy Money
Kuuza sura kwenye video za Kibongo ndipo kulipompa jina kisha akajiingiza kwenye muziki na utangazaji na kujiongezea umaarufu. Amekuwa miongoni mwa wauza sura wenye kusumbua mitandaoni kwa picha za mitego.
amber-lulu-na-kibonge-sexyAmber Lulu akiwa Global TV Online.
Amber Lulu
Amber naye amesumbua mwaka huu kwa picha tata. Ameshauza sura kwenye video kibao zikiwemo Inde ya Dully na Too Much ya Darassa. Bado anaendelea kusumbua na picha za mitego mitandaoni kutokana na dili anazopata za kutangaza nguo za ndani.
sanchoka-4Mhariri wa Gazeti la Championi Ijumaa, John Joseph (kushoto) akiwa na Sanchoka.
Sanchi
Figa na umbo lake limemfanya kuingia kati ya modo waliosumbua mwaka huu. Ukaribu wake na mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan umemfanya avume zaidi. Anaendelea kusumbua mitandaoni kutokana na picha zake za mitego.
KIDOA (5)Kidoa Salum.
Kidoa
Huyu ni Ijumaa Sexiest Girl mwaka jana. Tangu apate tuzo hiyo amekuwa akiandikwa kwa matukio mengi. Shepu yake imemfanya kutikisa kila akitupia picha mitandaoni. Ukaribu wake na Mwanasoka Mbwana Samatta umemfanya jina lake lizidi kukwea. Kwa sasa anaendelea kubamba na tamthiliya ya Huba.
lulu-diva-1Lulu Diva
Lulu Diva
Kuuza sura kwenye Video ya Naogopa ya Mirror akimshirikisha Baraka The Prince kulimuingiza katika chati ya wauza sura. Amesumbua kwenye video nyingine kibao kama Remix ya Burger Movie Selfie ya Belle9. Amejiingiza kwenye muziki na anafanya vizuri na Wimbo wa Milele akiwa na Barnaba.
Tunda
Amekuwa akisumbua mitandaoni kutokana na picha mbalimbali zikimuonesha akila bata katika hoteli kubwa za ndani na nje ya nchi. Uhusiano wake na msanii Young Dee umemuweka kwenye ramani nyingine huku video alizouza sura ikiwemo Salome ya Diamond zikimjengea heshima.
erycahErycah
Erycah
Moja kati ya video queen waliosumbua kwa picha katika mitandao ya kijamii. Mwaka huu nyota yake ilianza rasmi kujulikana kupitia Video ya Kwa Hela ya Linex na baada ya hapo akawa akiingiza dili nyingi za kutangaza mavazi.
lynnLynn
Lynn
Amevuma baada ya kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond na kupachikwa mimba. Ameng’ara kwenye video nyingi za wasanii wa Wasafi Classic Baby (WCB) kiasi cha kulifanya jina lake liwe juu.
Baby Nahiyyah
Alianza kufahamika kwa mara ya kwanza alipouza sura kwenye Video ya Siachani Nawe ya Barakah The Prince kisha Togola ya Dully. Ameendelea kutikisa hadi sasa kutokana na kupata michongo mingi ya kutangaza mavazi.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM