Friday, 16 December 2016

HATIMAYE Tunda Man Akiri Kuwa na Tofauti na Babutale...Adai Hali Hiyo Inamuumiza Sana

Tunda Man amefunguka sababu ilinayomfanya asielewane na bosi wake wa Tip Top Connection, Babutale.

Akiongea na EATV, muimbaji huyo wa ‘Mama Kijacho’ amesema, “Najutia kuwa na misunderstanding na bosi wangu. Kiukweli mimi na bosi wangu Babutale hatuko sawa, kosa silijui. Kuna kitu mimi nimemkosea may be au ameamua tu kukasirika na kiukweli hii kuwa mbali na bosi wangu kwenye kazi zangu ninazozifanya nakuwa mwenyewe tu kiukweli it’s pain, naumia.”

“Lakini sometimes mtu anaweza akawa na mwanae akamwambia nenda katafute maisha kivyake japo baba yake anakila kitu, kwahiyo unakuta mtoto anaondoka kutafuta maisha mengine, anabeba zege anafanyaje lakini anajutia kuwa mbali na baba yake. Lakini mimi najutia kwa sababu kazi zangu nakuwa na wakati mgumu wa kuzipush na kusupport kazi zangu lakini Alhamdulillah Mungu anasaidia.”

Tunda ameongeza kuwa kuna kipindi alipata dili la kufanya tangazo lakini kuna mtu alimpandia na nafasi hiyo akapewa msanii mwingine anayesimamiwa na Tale.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM