Saturday, 24 December 2016

FRANCIS CHEKA:KESHO SITAPANDA ULINGONI LEO SIJAMALIZIWA MALIPO YANGU


 Ameandika kupitia account yake ya facebook

Habarini za jioni mashabiki wangu poleni sanaa na majukumu Nipo Dar es Salaam Napenda kuwajurisha kesho SITAPANDA ULINGONI ifahamike hivyo na maamuzi haya nimeamua kwa kushirikiana na management yangu baada ya promota kutoonyesha ushirikiano.Ngumi ndio kazi yangu napigana ili nipate pesa sasa mtu anaandaa pambano halafu pesa ya kumlipa bondia ili apande ulingoni haijamaliziwa kwangu mpaka sasa na leo siku ya kupima uzito ndio ilitakiwa nimaliziwe malipo yang lakini hakuna kilichofanyika utaratibu wangu wa kazi huwa sipandi ulingoni bila kulipwa pesa yangu na huwa siupi nafasi ubabaishaji ktk kazi yangu.Kwa hiyo mashabiki wangu kama mtapenda mnaweza kujitokeza PTA kuwaona mabondia wengine watakaopanda ulingoni.Nawaombeni radhi mashabiki wangu nipo tayari kupigana kwa siku nyingine yoyote atakapomalizia malipo yangu.Nawatakieni sikukuu njemaa ya xmass na mwaka mpyaaa.Ahsanteni sanaa

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM