Monday, 12 December 2016

'Dume Suruali' ya Mwana FA na ‘Muziki’ ya Darassa Zachuana Vikali Youtube

Video ya ‘Dume Suruali’ ya Mwana FA akiwa na Vanessa Mdee pamoja na video ya ‘Muziki’ ya Darassa akiwa na Ben Pol ndizo video za muziki wa rap Tanzania zinazoongoza kwa kuangaliwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube kwa muda mfupi hivi sasa.
 
Video hizo zimeonekana kutoana nduki kwa mashabiki wao kuziangalia mara nyingi zaidi zikigusa rekodi ya kuangaliwa zaidi ya mara milioni moja ndani ya kipindi kisichozidi wiki mbili tangu zilipopandishwa mtandaoni.
 
Muziki ya Darassa imeshaangaliwa zaidi ya mara milioni 1.43 tangu ilipopandishwa kwenye mtandao huo Novemba 23 mwaka huu huku ‘Dume Suruali’ ikiangaliwa zaidi ya mara milioni 1.13 tangu ilipowekwa YouTube Novemba 25 mwaka huu. 
 
Hii inaonesha kuwa hivi sasa wasanii wanaungwa mkono zaidi na mashabiki wao kwa kuangalia video zao kwenye mtandao kutokana na uwepo wa mapinduzi ya kiteknlojia, ambapo mamilioni ya Watanzania sasa wanaweza kupata ‘internet’ kwenye simu zao.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM