Sunday, December 18, 2016

BREAKING NEWSS:MSANII DARASSA ANUSURIKA KIFO KWENYE AJALI YA GARI


 Muonekano wa gari alilopata nalo ajali ainaya Toyota Harrier

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mwanamuziki wa Hip Hop Bongo ambaye anasumbua na ngoma yake kali ya Muziki, Sharrif  Thabit ‘Darassa’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya maeneo ya Ntobo barabara ya kuelekea Mgodi wa Bullyanhulu Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Habari zimeeleza kuwa ndani ya gari hilo aina ya Toyota Harrier  ambalo dereva hajajulikana, Darassa alikuwa ameambatana na director wake, Hanscana pamoja na producer wake, Abba Process na wote wametoka salama.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Darassa amethibitisha kupata ajali hiyo na alipopigiwa simu na na mtandao huu alisema hawezi kuongea kwa sasa hivyo atafutwe baadaye.
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.