

Jana
team nzima ya WCB Wasafi na team ya XXL walikuwa pande za limani City
jijini Dar es Salaam kwenye tukio zima la kuuza tiketi kwaajili ya show
ya leo pande za Jangwani Sea Breez kwenye Wasafi Beach Party.
Wakali hao waliweza kukutana na mashabiki zao ana kwa ana na kuruhusu
maswali mawili matatu kutoka kwa mashabiki. Mmoja kati ya watu ambao
walipokea maswali kutoka kwa mashabiki ni pamoja na meneja wa Diamond
Platnumz mtu mzima Babu Tale.
Swali ambalo aliulizwa meneja huyo ilikuwa ni kuhusu rapper Chidi Benzi
ambaye tetesi za kitaa zinasema amerudi tena kwenye utumiaji wa madawa
ya kulevya ikiwa hapo awali meneja huyo allisikika kujitolea kumsaidia
rapper huyo.
“Chidi Benz nimemsaidia kwasababu mimi ni mtoto wa kiume na nimezaa
watoto wa kiume, lakini wanasemaga sikio la kufa halisikii dawa. Mimi
nimemsaidia lakini ikafika wakati nikashindwa kwasababu niliona mtu ndio
vile vile hajaacha ikanibidi nikae pembeni.”
Hayo ni baadhi tu kati ya mengi ambayo Babu Tale amefunguka kuhusiana na
Chidi Benz. Unaweza kumsikiliza yeye mwenyewe akifunguka mwanzo hadi
mwisho kwa kuplay hii video hapa chini.
No comments:
Post a Comment