Sunday, 18 December 2016

Alikiba ashiriki kwenye mechi ya soka ya hisani Uganda, atunukiwa tuzo

Kama isingekuwa muziki, huenda Alikiba angekuwa mmoja wa vinara wa timu kubwa za soka nchini, zikiwemo Simba au Yanga.
Baada ya mechi, Alikiba alitunikiwa tuzo ya mchezaji bora staa
Pamoja na kufanya muziki, Alikiba hutumia muda wake mwingine kujikumbushia kipaji chake cha soka, na ndio maana Jumamosi hii alishiriki mechi ya hisani ya mchezo huo jijini Kampala, iliyopewa jina ‘A Celebrity For Charity.’ Mechi hiyo ilichezwa kwenye uwanja wa Kabira Country Club na kuhusisha nyota wengine akiwemo Emmanuel Okwi.
Timu ya Alikiba na Okwi ilishinda mabao 4-1 huku Kiba akifunga bao la 2.
Alikiba akiwa na Jack Pemba na promota maarufu wa Uganda, Aly Allibhai
“We won the game!!! White KingKiba team 4 The Green Team 1
Second goal courtesy of your King. Thank you Uganda for the Award for Best Celebrity Player Award,” ameandika Alikiba kwenye Instagram.
Alikiba akiwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM