Saturday, 19 November 2016

Yule Mwanamume mwenye HIV aliyefanya mapenzi na wanawake 104 Malawi apatikana na hatia

Eric Aniva alifanya mapenzi na zaidi ya wanawake 100 licha ya kujua kuwa alikuwa na virusi vya HIV
Mwanamume mmoja raia wa Malawi aliye na virusi vya HIV amepatikana na hatia chini ya sheria ya jinsia ya nchi hiyo,baada ya kukiri kufanya ngono na wanawake 104 bila kufichua hali yake ya kiafya
Eric Aniva alikamatwa chini ya amri ya rais baada ya kukiri katika mahojiano na BBC kwamba, alishiriki ngono na zaidi ya wasichana 100 na wanawake pasipo kufichua kwamba aliugua virusi vya ugonjwa wa ukimwi . Kwa mujibu wa sheri za jinisia nchini humo
Mahakama moja imempata na hatia kwa kujihusisha katika kile ilichokitaja kuwa utamaduni wenye madhara, baada ya wanawake wawili kutoa ushahidi na kukiri kwamba jamaa huyo alilipwa na jamii kutekeleza tambiko ambapo mwanamume hulipwa kushiriki ngono na wajane walioanza kufiwa na waume zao.
Eric Aniva alifanya mapenzi na zaidi ya wanawake 100 licha ya kujua kuwa alikuwa na virusi vya HIVImage copyrightAFP
Image caption 
Utamaduni huo umepigwa marufuku chini ya sheria za Malawi. Aniva pia alikiri kwamba amelipwa kushiriki ngono na wasichana wadogo na kuendelea na hilo licha ya kutambua kuwa ana virusi vya HIV.
Kesi hiyo imeangaziwa katika vyombo vya habari vya kimataifa na imezusha mgawanyiko wa hisia kuhusu ni kwa ukubwa gani utamaduni huu umetapakaa.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM