Wednesday, 30 November 2016

YA WALIMWENGU:JAMAA APEWA TALAKA KUPITIA MTANDAO WA FACEBOOK

http://seeromega.com/wp-content/uploads/2016/09/facebook.jpg
Labda tunajisifu kuwa tuko kwenye ulimwengu ambao teknolojia imerahisisha vingi.. unahitaji kuwasiliana na mtu yuko mbali.. Viber, Facebook, Twitter zinasaidisa yaani kirahisi kabisa.

Kutokana na Sheria za nchi kuwa tofauti, hii story ya Marekani kuruhusu mtu kuomba talaka kwa kutumia message ya Facebook imenishtua kidogo.
Ishu ilianzia utata ulioanza mapema kabisa Ellanora Baidoo alipofunga ndoa ya kimila mwaka 2009 na mpenzi wake  Victor Sena Blood-Dzraku, lakini uhusiano wao ukawa kama umevunjika; bwana anaishi mahali ambako bibi hapajui, mawasiliano yao ni Facebook basi !!
Bibi akaona isiwe taabu, akaenda Mahakamani kuomba Mahakama impe ruhusa aombe talaka yake kupitia message ya Facebook kwa kuwa ndio njia pekee ambayo walikuwa wakitumia kuwasiliana.
Jaji wa Mahakama ya Manhattan aliruhusu bibi huyo abadilishe status yake, aweke #single halafu huyo bwana afikishiwe ujumbe wa kudai talaka kupitia message ya Facebook, ambayo toka message hiyo imetumwa jamaa hakujibu.
Wakili wa mwanamke huyo Andrew Spinnell amefurahishwa na uamuzi huo wa Mahakama, anaamini kwa sasa kuna haja ya kutumia hata hizi social networks kutoa hukumu kama ilivyofanywa kwa mume wa Baidoo.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM