Tuesday, November 8, 2016

Wezi waiba hela na kutoweka na mtambo wa ATM

Polisi nchini Kenya katika jiji kuu Nairobi wamemkamata mlinzi wa Benki ya Equity kuhusiana na wizi mwishoni mwa wiki ambapo wezi walitoweka na mtambo wa kutoa pesa, ATM. atm-machine
Wezi hao walitoweka na kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana kwa sasa wakati wa wizi huo Jumamosi.
Wezi hao walichimba ukuta wa nyuma wa Benki hiyo na kutoweka na sanduku la uhifadhi wa pesa pamoja na mtambo wa ATM, pesa zikiwa ndani.
Washukiwa waliweza kuzima kamera za CCTV na pia kengele ya usalama kabla ya kutekeleza wizi huo.
Akizungumza na BBC, kamanda wa jimbo la Nairobi Japheth Koome amesema kwamba polisi waliweza kupata mitungi ya gesi na vifaa vingine ambavyo hutumuka kukata chuma.
Alipoulizwa kama wezi siku hizi wamepata umaarifa utadhani wanaiga filamu, alisema kwamba kwa siku za hivi karibuni wizi wa benki unazidi kubadilika sana.
Mwaka uliopita, wezi waliojifanya wakaguzi wa hesabu katika benki hiyo walitoweka na dola za Marekani 300,000.
BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

Total Pageviews

BONYEZA HAPO CHINI

TAZAMA FRANCIS CHEKA TV

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.